ROSE NDAUKA ATAKA VIJANA WAWE MAKINI NA UCHAGUZI 2015



ROSE NDAUKA ATAKA VIJANA WAWE MAKINI NA UCHAGUZI 2015

MSANII nyota wa filamu za kibongo Rose Ndauka, amesema kuwa pamoja na kuwa vijana ndiyo wenye nguvu ndani ya taifa lolote duniani lakini wanatakiwa kuwa makini kipindi hiki cha kuelekea cha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanya Oktoba mwaka huu.
Ndauka alizungumza na mtandao huu na kusema kuwa, suala linaloweza kutokea ni kwamba vijana wanaweza kutumika vibaya bila wenyewe kujua, lakini hiyo haitaweza kuwasaidia zaidi ya kuwaharibia.
"Kupiga kura ni wajibu lakini vijana wanapaswa kujua wanatumikaje, ni lazima wawe makini ili kuilinda nchi yetu na kuwaepuka wale viongozi wanaotaka madaraka kwa njia isiyofaa," alisema Ndauka.


Comments