Wakuu, wakati najipanga kumpa pongezi Madam Anna kwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa kuchaguliwa ACT, nimeshitushwa na mijadala inayoendelea kwenye mitandao kuhusu kifungu kilichobadilishwa jana kikiweka nafasi ya kiongozi mkuu wa Chama.
Kilichonistua zaidi ni nguvu aliyopewa kiongozi mkuu wa Chama, mpaka anaitwa nuru ya Chama? Halafu nasikia nafasi hii haikugombaniwa na Zitto ndiye kiongozi mkuu wa Chama. Labda nimemezeshwa sumu maana sikuamini nilipoona hivyo vipengele. Wenye taarifa watujuze na kifungu hiki kimekaaje? Kwa nguvu aliyopewa kiongozi mkuu, Yaani kina madam Anna wako kama viraka tu?
Ebu tuangalie kazi za kiongozi mkuu na kisha tafuta ya mwenyekiti.
"Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania
i) Atakuwa kiongozi mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa,
mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.
ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na
maafisa wa ACT-Tanzania
iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii
iv) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa
chama
v) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu
na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa
na kimataifa.
vi) Atasimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-
Tanzania
vii) Iwapo kiongozi wa ACT-Tanzania hayupo kwa sababu yoyote ile basi
Mwenyekiti wa chama Taifa atakuwa Kaimu kiongozi mkuu wa Chama.
viii) Iwapo kiti cha kiongozi mkuu wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya
kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama,
maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu
ulioelezwa katika (vi) ya ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba
Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi
sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi Mkuu
wa Chama mwingine.
ix) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa
litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya kura za wajumbe halali
waliohudhuria na kupiga kura.
x) Atakuwa ni nuru na taswira ya ACT-Tanzania"
Comments
Post a Comment