CUF YATAKA WAZIRI TAMISEMI, MKURUGENZI KINONDONI WAJIUZULU



CUF YATAKA WAZIRI TAMISEMI, MKURUGENZI KINONDONI WAJIUZULU
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, Magdalena Sakaya, akizungumza na wanahabari(hawapo pichani).
Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini katika mkutano wa CUF.Moja ya majengo ya ofisi za CUF jijini Dar.
KUFUATIA kuibuka kwa fujo na adha mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini, kuanzia zoezi la upigwaji wa kura mpaka uapishwaji wa wenyeviti hao kuzua utata, Chama cha Wananchi (CUF) leo kimewataka Waziri wa Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kinondoni na kujiuzulu kwa vile wameshindwa kuendesha  uchaguzi huo.
Aidha Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, Magdalena Sakaya, ametaja baadhi ya maeneo yaliyogubikwa na fujo hizo katika uapishwaji wa wenyeviti kuwa ni pamoja na  Kawe, Kinondoni, Mwananyamala, Kiwalani, Buguruni, Kinyerezi, Migoba, Kigogo na kwingineko.


Comments