VIJANA wametakiwa kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam jana, na mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Saranga Kata ya Kimara, Edwin Agola (CHADEMA) alipokuwa akirejesha fomu.
Agola alisema vijana wengi wamekuwa wakipuuza kugombea nafasi hizo za ngazi ya kitongoji na mtaa wakidhani wanaotakiwa kufanya hivyo ni wazee.
"Unajua vijana wengi wanapuuza kugombea nafasi hizi kwa sababu wanaamini unapokuwa mwenyekiti wa kitongoji au mtaa kazi kubwa ni kushughulika na utatuzi wa migogoro ya ndoa na masuala ya kimila huku wakiamini umri wao sio wakufanya kazi hiyo,"alisema Agola.
Alisema umefika wakati kwa vijana kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi hizo, wakitambua kuwa nafasi hizo ni muhimu kwani huko ndiko kwenye wananchi wengi ambao wanahitaji watetezi wa kweli katika haki zao.
Comments
Post a Comment