UKAWA wanyaka nyaraka juu ya Mpango wa kifisadi wa kupitisha Katiba Inayopendekezwa


UKAWA wanyaka nyaraka juu ya Mpango wa kifisadi wa kupitisha Katiba Inayopendekezwa Wakati wananchi wanalazimika kujichangisha fedha zao mifukoni ili wapate huduma pale Hospitali ya Muhimbili kwa sababu Serikali imeshindwa kuilipa MSD, Serikali ya CCM inapanga mipango ya hila ikitumia mabilioni kurubuni Watanzania waipitishe Katiba Inayopendekezwa!

Leo UKAWA wanahoji, haya mabilioni ambayo Rais Kikwete ameagiza kwenye mpango huu akiwa ndani ya ndege, yameidhinishwa na kikao kipi cha bunge? Yako kwenye Kasma ipi ya bajeti? Tangu lini fedha za walipa kodi maskini zikatumika kwa ajili ya kuiepusha CCM na aibu ya kura ya HAPANA?

Soma kwa makini mkakati mzima huu hapa kama ulivyoanikwa leo na viongozi wakuu wa UKAWA, walipokutana na waandishi Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha CUF.





Comments