Kwanza Halima Mdee alikamatwa. Pili Halima Mdee akaachiwa kwa dhamana ya Polisi. Tatu Halima Mdee alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yake. Nne, upande wa Mashtaka haukuwa na pingamizi juu ya dhamana ya Halima Mdee wala wenzake. Tano,Hakimu akatoa masharti ya dhamana. Sita, washtakiwa wote walikuwa tayari kuyatekeleza na kuachiwa kwa dhamana. Saba, upande wa Mashtaka ukataka kwenda kuhakiki wadhamini wa Halima Mdee na wenzake.
Umepagundua penye tatizo? Ni hapo pa kuhakiki wadhamini. Halima Mdee anajulikana. Wadhamini wake, ambao wengi ni Wabunge na Maafisa wa CHADEMA Makao Makuu wanajulikana. Kuhakiki kulikujaje? Wengine mbona hawafanyiwi hivyo? Kibaya zaidi,wahakiki hawakuenda mahali popote hadi Halima Mdee alipopandishwa karandinga na kwenda mahabusu. Wahakiki walitokomea kusikojulikana. Why?........Kwanini?
Nitoe rai kwa wahusika wote kufanikishadhamana ya Halima Mdee. Ingawa si wachama changu, hastahili kombolela lililochezwa jana. Hakuna haja ya 'kuipaisha' CHADEMA na viongozi wake kupitia Mahakama. We are suffering from that;it must end! Pole sana Halima Mdee.

Comments
Post a Comment