Jaji Warioba: Siendi Ng'o Dodoma Kwenye Makabidhiano ya Katiba



Jaji Warioba: Siendi Ng'o Dodoma Kwenye Makabidhiano ya Katiba
Wakati Katiba inayopendekezwa ikikabidhiwa kesho kwa Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hata akialikwa katika sherehe hizo hatahudhuria kutokana na majukumu aliyonayo kwa sasa.

Jaji Warioba alisema angependa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo pia itahudhuriwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wakuu wa mikoa, mabalozi na wageni mbalimbali, lakini kutokana na dharura aliyoipata haitawezekana.

Sherehe hiyo itafanyika mkoani Dodoma kesho na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta atakabidhi nakala ya Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, wajumbe wa Bunge hilo walioshiriki mchakato huo kuanzia mwanzo mpaka mwisho watapewa vyeti.

Comments