Nanyaro anagombea Uwenyekiti wa BAVICHA Taifa

Namshukuru sana Mwenyenzi Mungu kwa wingi wa neema na rehema zake.Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa moyo wa dhati kabisa viongozi wa BAVICHA Taifa  wanaomaliza muda wao(John Heche Mwenyekiti  na Deo Munish Katibu Mkuu)nawapongeza kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya na leo BAVICHA ni taasisi kubwa na imara.Pia nawapongeza wote waliochaguliwa kuongoza BAVICHA kuanzia ngazi za misingi,matawi,kata,Wilaya na Mikoa.

Mimi Ephata Nanyaro nimezaliwa  tarehe 27.11.1984,nina mke mmoja na watoto wawili.Elimu yangu ni shahada ya kwanza

UZOEFU WA KIUONGOZI NDANI YA CHAMA

-Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Arusha(2009-2014)

-Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Arusha mjini(2011-2014)

-Diwani wa kata ya Levolosi Arusha Mjini(2010-2015)

_Mmoja wa waanzilishi wa VIPATU  taasisi ya vijana ambayo imeinua vijana wengi Kiuchumi mkoa wa Arusha

KWA NINI NAFAA KUWA MWENYEKITI

 

               1.Uwezo wa kiuongozi

Nimekiongoza chama wilaya ya Arusha mjini kwa mafanikio makubwa sana,katika kipindi cha uongozi wangu tulifanikiwa kushinda chaguzi zote ndogo,na kata ya Sombetini na Daraja mbili ambazo awali zilikuwa ccm tukazirejesha CHADEMA.Nimewatumikia wanawanchi wangu wa Levolosi kwa uaminifu na uwezo mkubwa,ambapo tumeweza kutekeleza ahadi zetu kwa 80% hadi sasa.

 

2.Ubunifu

Tumebuni miradi mbalimbali ya BAVICHA Mkoa wa Arusha,yenye malengo ya (a)Kuboresha na kuinua maisha ya vijana kiuchumi(b)Kukifanya chama kuwa relevant kwa wananchi wengi.Chini ya mpango huu tulianzisha VIPATU(Vijana pamoja tunaweza)

 

3.Oganizesheni imara ya BAVICHA

Kwa kuwa malengo makuu ya chama ni kuchukua DOLA,na BAVICHA ina jukumu kubwa la Kuhakikisha malengo makuu ya chama yanafikiwa.Hivyo tunahitaji kujenga oganaizesheni imara ya BAVICHA kutoka chini hadi juu.BAVICHA itakayokuwa mhimili mkuu wa CHAMA katika kufikia malengo,hili tutalijenga katika misingi ya Uadilifu,Uwajibikaji,Uwazi,Utu na Ujasi ri mkubwa sana  

 

 

 

Kwa heshima sana naomba KURA kwa  vijana wenzangu,wajumbe wote wa mkutano mkuu wa BAVICHA,na wasio wajumbe ninawaomba sana mniunge mkono katika kuwatumikia vijana .Hakika ukinichagua hutoijutia kura yako.

CHAGUA NANYARO BAVICHA 2014-2019

Kuhakikisha BAVICHA inafanikisha malengo ya CHADEMA
.Kuhakikisha dira kuu ya BAVICHA  inafikiwa yaani vijana kuwa nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla
.Kuwezesha sera sahihi,uongozi bora na kujenga oganizesheni dhabiti ya
vijana kwa maendeleo endelevu
.Mafunzo ya maswala ya kijamii(afya,uchumi,demokrasia,na uongozi)
.Chemichemi ya uongozi

“And there comes

A time when one must take a position that is neither safe, nor politic, nor popular but he/she must do it because CONSCIENCE tells him it is RIGHT” Ephata Nanyaro BAVICHA 2014-2019


-- 

Ephata Nanyaro
P.o.box 15359
Arusha
+255 754 834152
Skype.nanyaro.ephata

"truth shall set you free"


Comments