Mahakama ya Afrika Mashariki yatoa hukumu kuwa uchaguzi wa wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki ulikua batili
Mahakama ya Afrika Mashariki imesema uchaguzi wa wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki ulikua batili kutokana na kukiukwa kwa ibara ya hamsini ya mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Jaji kiongozi wa mahakama hiyo Jean Bosco Butasi akiwa na majaji wengine wa mahakama hiyo Isaac Lenaola na jaji Faustine Ntezilyayo wametoa uamuzi huo katika hukumu ya kesi iliyofunguliwa na aliyekua mmoja wa wagombea wa ubunge wa bunge hilo la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Bwana Antony Komu kutoka Chadema.
Katika hukumu hiyo ya kurasa thelathini na nane, mahakama hiyo imempa ushindi komu katika hoja zake zote tatu na kutupilia mbali pingamizi la mwanasheria mkuu wa serikali katika kesi hiyo na hivyo kuitaka serikali kulipa gharama za kesi hiyo.
Madai ya msingi ya Bwana Komu katika kesi hiyo ya shauri namba saba la mwaka 2012 yalikua ni kupinga utaratibu uliotumika kupata wagombea wa bunge ambao alieleza kuwa haukuzingatia uwiano ambapo pia alihoji uhalali wa Chadema kama chama kikuu cha upinzani chenye kuunda baraza kivuli kukosa uwakilihsi bungeni humo.
Bwana Komu na wakili wake John Mallya pamoja na mbunge wa jimbo la Arusha mjini wamezungumzia hukumu hiyo.
Hata hivyo mahakama hiyo imesema haina mamlaka ya kuwaengua wabunge waliopo hivyo kesi hiyo inapaswa kuwasilishwa kwenye mahakama kuu Dodoma hatua ambayo mlalamikaji na wakili wake wamesema itachukuliwa haraka.
Comments
Post a Comment