Jaji Warioba: Bunge lisitishwe Katiba Mpya Haiwezi Patikana Ndani ya Wiki Mbili zilizobakia



ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema ni vyema Bunge Maalumu la Katiba likasitishwa kwani Katiba bora haiwezi kupatikana kwa muda wa wiki mbili.


Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku moja baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kumtaka Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kulisitisha, huku mwenyewe akisema litaendelea na hadi kufikia Oktoba 4 Katiba inayopendekezwa itapatikana.

Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwa haraka waliyokuwanayo wajumbe wa Bunge hilo 

wakati wanajua kuwa Katiba haiwezi kupatikana kwa muda uliobaki.

Alisema wiki mbili au tatu zilizobaki ni chache mno na kwamba Katiba mpya haiwezi kupatikana, hivyo ni vyema sasa busara ikatumika kulisitisha.

"Mimi sizungumzii kauli ya Ukawa, lakini natoa maoni yangu kwamba sidhani kama watamaliza kwa kipindi hiki kifupi, kuna mambo hawawezi kupata kwa muda huu mfupi.

"Ninachotaka watumie tu busara waliahirishe… sijui haraka yao hii ni ya nini. Kwanini wanashindwa kuelewa kuwa Katiba ni suala la maridhiano?" alihoji Jaji Warioba.

Comments